News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

‘KIVUMBI’ CHA LIGI KUU YA NBC KUANZA LEO.

PAZIA la Ligi kuu ya NBC msimu wa 2023/2024 linafunguliwa rasmi leo Agosti 15 kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja mbalimbali. Mchezo wa kwanza wa ufunguzi utazikutanisha Ihefu dhidi ya Geita Gold saa 10:00 alasiri katika uwanja wa Highland Estate, Mbeya mchezo wa pili utazikutanisha Namungo dhidi ya JKT Tanzania saa 12:30 usiku katika Uwanja…

Honest Mwanitega · Read more

SIMBA BINGWA MPYA WA NGAO YA JAMII.

Baada ya timu ya Yanga kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii kwa miaka miwili mfululizo hatimaye timu ya Simba Leo Agosti 13, 2023 imefanikiwa kushinda mchezo wa fainali na kutwaa ubingwa huo. Simba wametwaa ubingwa huo kwa kuifunga Yanga Kwa mikwaju ya penati 3-1 ikiwa ni baada ya mchezo huo kumalizika kwa suluhu ndani ya…

Honest Mwanitega · Read more

NI KARIAKOO ‘DERBY’ FAINALI NGAO YA JAMII.

TIMU ya Simba imefanikiwa kufuzu fainali ya Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Singida Big Stars baada ya kumalizika kwa suluhu ndani ya dakika 90. Simba itakutana na Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwa mara ya tatu mfululizo huku ikiwa imefungwa katika mara zote mbili zilizopita. Penati zilizofungwa na…

Honest Mwanitega · Read more

YANGA YATANGULIA FAINALI NGAO YA JAMII.

TIMU ya Yanga imefanikiwa kufuzu fainali ya Ngao ya Jamii baada ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Azam katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Azam iliyokuwa imejichimbia nchini Tunisia kwa maandalizi ya msimu mpya imeshindwa kutamba na kuruhusu mabao hayo mawili yaliyofungwa na Stephane Aziz Ki na Clement Mzize walioingia kipindi cha pili. Matokeo hayo yanaifanya…

Honest Mwanitega · Read more

LIGI KUU RASMI AGOSTI 15.

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/2024 utakaoanza Agosti 15, na kutamatika Mei 29, 2024. Michezo ya ufunguzi itaanza Agosti 15 ikiwakutanisha Ihefu na Geita Gold uwanja wa Highland Estate, Namungo na JKT Tanzania uwanja wa Majaliwa na Dodoma Jiji dhidi ya Coastal Union uwanja wa…

Honest Mwanitega · Read more

KASONGO AWAITA MADAKTARI VIWANJANI

AFISA Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Almasi Kasongo ameushauri uongozi wa Chama cha Madaktari wa Michezo nchini (TASMA) kutengeneza mazingira rafiki yatakayovutia madaktari wengi zaidi wanaofanya kazi katika Hospitali mbalimbali. Amesema hayo alipokuwa akifungua Semina ya madaktari wa michezo inayofanyika Mkoani Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano katika uwanja wa Benjamin…

Honest Mwanitega · Read more

RATIBA ZA MASHINDANO ZATAMBULISHWA.

BODI ya Ligi Kuu Tanzania imetangaza tarehe za matukio yote ya msimu mpya wa 2023/24 ikiwa ni pamoja na siku za kuanza kwa Ligi Kuu ya NBC, Championship na First League. Ligi Kuu ya NBC inatarajiwa kuanza Agosti 15 ikitanguliwa na michezo ya Ngao ya Jamii itakayochezwa mkoani Tanga kuanzia Agosti 9 mpaka Agosti 13…

Honest Mwanitega · Read more

HAWA HAPA NYOTA WAPYA LIGI KUU YA NBC.

DIRISHA la usajili msimu mpya wa 2023/24 kwa klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake lilifunguliwa Julai Mosi ili kuruhusu timu kuhamisha wachezaji kutoka timu moja Kwenda nyingine. Timu mbali mbali za Ligi Kuu zimeendelea kujiimarisha kwa kutangaza wachezaji na makocha watakaowasimamia katika michezo yao kuelekea msimu…

Honest Mwanitega · Read more

JKT, KITAYOSCE, MASHUJAA NA LADHA MPYA LIGI KUU.

TIMU za JKT Tanzania ya Dar es Salaam, Kitayosce ya Tabora na Mashujaa ya Kigoma zimefanikiwa kupanda Ligi Kuu Ya NBC msimu wa 2023/24 huku kila mmoja akiwa na rekodi zake mpaka kufikia hatua hiyo. JKT ilifanikiwa kupanda Ligi Kuu baada ya kushinda michezo mingi zaidi (20) ikikusanya alama 63 na kuizidi timu ya Kitayosce…

Honest Mwanitega · Read more