News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

KMC YANG’ANG’ANIA KILELENI LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC.

LIGI ya Championship ya NBC 2026/2027 imeendelea kushika kasi ikiwa ni mzunguko wa tisa wa ligi hiyo huku timu zote 16 zikiwa zimeshiriki kikamilifu katika viwanja tofauti ili kujitafutia alama kwenye mizunguko yote. KMC ya Dar es Salaam inaongoza msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa imecheza michezo tisa bila kupoteza mchezo wowote. KMC…

Loveness Bernard · Read more

GUEYE HAKAMATIKI KWENYE SUALA LA KUPIKA MABAO LIGI KUU NBC.

Kiungo wa Simba SC, Libasse Gueye, anaendelea kung’ara katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027, akiongoza orodha ya wachezaji wenye pasi nyingi za mwisho zilizozaa mabao (assists), akiwa amefikisha jumla ya pasi saba za mabao. Gueye amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaoonyesha ubora mkubwa katika kutengeneza nafasi za kufunga, akionyesha uwezo wa kulitazama vizuri lango…

Loveness Bernard · Read more

MPANZU,BARKER WANG’ARA TUZO ZA OKTOBA

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Elie Mpanzu amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2026/27, huku Steven Barker pia wa Simba akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo. Mpanzu alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiwashinda Iddi Selemani wa Azam FC na Nathaniel Chilambo wa…

Loveness Bernard · Read more

ANUARY HASHIKIKI UFUNGAJI BORA LIGI KUU YA NBC.

MSHAMBULIAJI Anuary Jabiri wa Polisi Tanzania ameendelea kung’ara katika mbio za kuwania kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027, akiwa kinara wa orodha hiyo kwa sasa kwa kufikisha mabao saba. Jabiri amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu, akijitengenezea nafasi ya kuongoza orodha ya wafungaji akiwa amecheza michezo tisa sawa na…

Loveness Bernard · Read more

HAMDANI KINARA WA MABAO LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC.

MCHUANO wa kuwania ufungaji bora katika Ligi ya Championship ya NBC msimu wa 2026/2027 inaendelea kushika kasi huku kila mchezaji akipambana kuhakikisha anafunga na kuisaidia timu yake. Mshambuliaji Hamdani Ally wa Transit Camp anaongoza orodha hiyo ya wafungaji bora baada ya kuweka nyavuni mabao tisa ndani ya mizunguko nane ambayo timu yake imeshacheza hadi sasa…

Loveness Bernard · Read more

SIMBA, TRA UNITED NA MASHUJAA ZAIBUKA NA USHINDI LIGI KUU YA NBC.

Ligi Kuu ya NBC msimu wa wa 2026/27 iliendelea kutimua ‘vumbi’ kwa timu za Simba, TRA United na Mashujaa baada ya kushinda michezo yao wakiwa uwanja wa nyumbani. Katika mchezo wa mapema uliochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid TRA United ilibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Fountain Gate. TRA united ilipata mabao…

Cynthia Michael · Read more

POLISI, YOUNG AFRICANS WAMALIZA WIKI VEMA LIGI KUU YA NBC.

Polisi Tanzania imepata ushindi wa kwanza msimu huu kwenye uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro dakika za mwisho baada ya kuifunga Geita Gold bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC. Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo ilibidi kusubiri hadi dakika za nyongeza Isaya Kuzoza wa Geita Gold kujifunga na kuipa Polisi Tanzania ushindi wa…

Cynthia Michael · Read more