News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

MABINGWA WAWILI ‘KUKIWASHA’ LEO AZAM COMPLEX.

LIGI Kuu ya NBC inaendelea leo Agosti 29 kwa mchezo mmoja kati ya Yanga na JKT Tanzania kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku. Mchezo huu unaikutanisha Yanga iliyokuwa bingwa wa Ligi Kuu NBC msimu uliopita na JKT iliyokuwa bingwa wa Ligi ya Championship msimu uliopita. Timu hizo zinacheza mchezo…

Honest Mwanitega · Read more

AZAM FC YAKAA KILELENI NBCPL.

TIMU ya Azam imepanda mpaka nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuifunga Prisons ya Mbeya kwa mabao 3-1. Mabao ya Prince Dube, Iddy Selemani na Nathaniel Chilambo yameifanya Azam kushika nafasi ya kwanza na kuwa timu kinara wa kufunga mabao (7). Ligi Kuu ya NBC itaendelea tena Agosti 29…

Honest Mwanitega · Read more

YANGA YAENDELEZA UBABE.

TIMU ya Yanga imeanza Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar kwa kishindo baada ya kuifunga KMC mabao 5-0. Dickson Job, Ki Aziz, Hafiz Konkoni, Midathir Yahya, na Pacome Zouzoua ndio walioifanya timu ya Yanga kuwa timu iliyofunga mabao mengi katika mchezo mmoja mpaka sasa katika Ligi Kuu ya…

Honest Mwanitega · Read more

GEITA YATAMBA UGENINI.

TIMU ya Geita Gold imeendelea kung’ara ikicheza ugenini baada ya kupata suluhu dhidi ya Mashujaa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. Geita imeanza vema Ligi Kuu ya NBC kwa kukusanya alama nne katika michezo miwili bila kuruhusu bao lolote tofauti na msimu uliopita waliporuhusu mabao manne katika michezo miwili ya mwanzo. Mashujaa iliyopanda daraja msimu…

Honest Mwanitega · Read more

SIMBA YAENDELEA ILIPOISHIA, MTIBWA, COASTAL HAKUNA MBABE.

TIMU ya Simba imepata ushindi wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji kwa mabao 2-0 na Kukwea kileleni mwa msimamo kwa mara ya kwanza msimu huu. Dodoma iliyoanza Ligi vema msimu huu kwa kuifunga Coastal Union mabao 2-1 imeshindwa kutamba mbele ya ‘Mnyama’ kwa mabao yaliyofungwa na Jean Baleke kipindi…

Honest Mwanitega · Read more

KAGERA NA MKOSI WA MSIMU ULIOPITA

TIMU ya Kagera Sugar imeendeleza rekodi mbaya ya mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufungwa bao 1-0 na Ihefu ya Mbeya. Kagera Sugar tayari imepoteza michezo miwili msimu huu dhidi ya Mashujaa na Ihefu idadi sawa na michezo miwili ya mwanzo msimu uliopita ilipofungwa na timu za Azam na Simba. Bao…

Honest Mwanitega · Read more

SIMBA YANGURUMA MANUNGU.

TIMU ya Simba imeanza Ligi Kuu ya NBC kwa kishindo baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 4-2 kwenye uwanja wa Manungu, Morogoro. Msimu uliopita Jean Baleke aliifunga Mtibwa mabao matatu na leo ameendeleza ubabe kwa timu hiyo baada ya kufunga bao moja huku mabao mengine yakifungwa na Fabrice Ngoma, Esomba Onana na Clatous Chama. Mabao…

Honest Mwanitega · Read more

MASHUJAA YAANZA LIGI KUU KISHUJAA.

TIMU ya Mashujaa ya Kigoma iliyopanda Ligi Kuu ya NBC ikitokea Ligi ya championship imeanza kibabe baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar. Mashujaa ilipata mabao yake kupitia kwa Adam Adam dakika ya 15 na Othman Dunia dakika ya 73 kwa mashuti yaliyopigwa kwa mguu wa kushoto. Timu ya Kagera imepoteza…

Honest Mwanitega · Read more

PAZIA LA LIGI KUU YA NBC LAFUNGULIWA

Baada ya siku 76 kupita Ligi Kuu ya NBC imerejea tena kwa michezo mitatu iliyochezwa viwanja vya mikoa mitatu tofauti na kushuhudia mabao matano yakifungwa kwa ujumla. Elias Maguli amekuwa ndiye mchezaji wa kwanza kufunga bao katika msimu huu wa 2023/24 na kuifanya timu ya Geita Gold kupata ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi…

Honest Mwanitega · Read more