News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

WALINDA ‘LANGO’ WANAOTIKISA LIGI YA CHAMPIONSHIP YA NBC.

Mzunguko wa 10 wa Ligi ya Championship ya NBC umetamatika huku Mtibwa Sugar ikiwa kinara wa Ligi hiyo. Hawa hapa walinda lango wanaoongoza orodha ya hati safi katika msimu wa 2026/27 ndani ya ligi hiyo hadi sasa; Abubakar Omari wa Bandari Tanzania ya mkoani Mtwara anaongoza orodha hiyo akiwa na hati safi sita. Kipa huyo…

Loveness Bernard · Read more

HAWA HAPA WALINZI WAKALI WA PASI SAIDIZI ZA MABAO LIGI KUU YA NBC.

MBIO za mafanikio ya timu ndani ya msimu wa 2026/2027 wa Ligi Kuu ya NBC zinanogeshwa na uwezo wa mabeki wa timu mbalimbali kuhusika katika mabao na sio kuzuia pekee. Hawa hapa wakali wa kutoa pasi saidizi za mabao kwa timu zao msimu huu hadi sasa; Salum Khamis wa JKT Tanzania anaongoza kwa pasi saidizi…

Loveness Bernard · Read more

FIRST LEAGUE KUNDI B ‘VITA’ IMEANZA MAPEMA .

Mzunguko wa tatu wa First league kundi B umetamatika kwa michezo minne huku Kigoma FC ikiendelea kuwa moto wa kuotea mbali. Kigoma imeendelea kushika usukani wa msimamo ikiwa imecheza michezo mitatu akiwa na alama tisa na akifunga mabao nane na kuruhusu bao moja, timu hiyo kutoka mkoani Kigoma imeshinda michezo yote hadi sasa. Madini…

Cynthia Michael · Read more

FIRST LEAGUE, KUNDI A KWA MOTO MSIMU HUU.

Mzunguko wa tatu wa First League umetamatika kwa michezo nane ambapo kundi A ni michezo minne na B ni michezo minne kwa mzunguko mmoja. Kinara wa Kundi A ni Cosmopolitan akiwa amecheza michezo mitatu ushindi mbili na kufungwa mchezo mmoja huku timu hiyo ikifunga mabao matano na kufungwa mabao mawili na kukusanya alama sita.…

Cynthia Michael · Read more

MTIBWA YAONGOZA ‘VITA’ YA UBINGWA NBC CHAMPIONSHIP.

LIGI ya Championship ya NBC msimu wa 2026/2027 inaendelea huku ushindani mkali ukiendelea baada ya timu zote kucheza mizunguko 10, huku Mtibwa Sugar ikishika usukani wa ligi hiyo kwa kukusanya pointi 21. Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro imejikusanyia alama hizo baada ya kushinda michezo sita, kutoka sare tatu na kupoteza mchezo mmoja, ikiwa imefunga mabao…

Loveness Bernard · Read more

LIBASSE KAHUSIKA MABAO MENGI LIGI KUU YA NBC.

Kiungo wa timu ya Simba, Libasse Gueye, anaendelea kuonyesha ubora wake katika msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuhusika katika mabao mengi kuliko mchezaji yoyote ndani ya Ligi hiyo. Gueye anaongoza akiwa amehusika katika mabao tisa, ambapo amefunga mabao mawili na kutoa pasi saidizi saba ndani ya mizunguko 10 ya Ligi…

Loveness Bernard · Read more

KARIA: MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YAMEONGEZA UBORA WA LIGI KUU YA NBC.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema ubora wa Ligi Kuu ya NBC umeendelea kuimarika kutokana na matumizi ya teknolojia mbalimbali, ikiwemo mfumo wa Football Video Support (FVS), ambao umesaidia kupunguza malalamiko yanayohusu maamuzi ya waamuzi. Karia ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa 13 wa Bodi ya Ligi Kuu…

Cynthia Michael · Read more

SIMBA ‘HAIFUNGIKI’ LIGI KUU YA NBC

LIGI Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027 ilianza tarehe 14 Agosti ambapo timu tofauti zilikutana katika viwanja tofauti na kuonyesha umahiri wao, huku Simba ikiwa timu pekee iliyoshinda michezo kumi mfululizo hadi sasa. Mechi yao ya kwanza kwenye msimu huu ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Agosti 16 kwenye uwanja wa Kaitaba uliopo Kagera ambapo…

Loveness Bernard · Read more

ANUARY MKALI WA MIKWAJU YA PENATI LIGI KUU YA NBC

MSHAMBULIAJI wa timu ya Polisi Tanzania Anuary Jabiri hashikiki kwenye kufunga mabao ya mkwaju wa penati ndani ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027. Mkali huyo amefunga mabao manne ya mkwaju wa penati katika mechi za Polisi Tanzania dhidi ya Azam katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, Polisi Tanzania dhidi ya Pamba Jiji,…

Loveness Bernard · Read more