News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

LADHA YA LIGI KUU YA NBC KUREJEA LEO

BAADA ya siku 15 kupita kupisha kalenda ya FIFA ya michezo ya kimataifa, Ligi Kuu ya NBC inarejea tena Leo Septemba 15 kwa michezo mitatu kuchezwa kwenye mikoa tofauti. Mchezo wa mapema utachezwa Saa 8:00 mchana kati ya KMC na JKT Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es salaam huku timu zote mbili zikipoteza kwenye…

Yahaya Abushehe · Read more

POLISI KUJIULIZA KWA RUVU, PAMBA, PAN KUKIWASHA LEO.

Ligi ya NBC Championship itaendelea leo Septemba 15 kwa michezo miwili kuchezwa kwenye mikoa ya Kilimanjaro na Mwanza. Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro saa 8:00 mchana huku mchezo huo ukitarajiwa kutangazwa Mbashara kupitia chaneli ya TV3. Baaada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Cosmopolitan kwenye mchezo…

Yahaya Abushehe · Read more

NBC CHAMPIONSHIP LIVE TV3

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo Septemba 13 wameingia mkataba wa miaka mitatu (3) wa haki za matangazo ya televisheni kwa ligi ya NBC Championship na TV3 wenye thamani ya shilingi Milioni 613 kuanzia msimu wa 2023/2024 mpaka 2025/2026. Akizungumza wakati wa hafla ya makubaliano hayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu…

Yahaya Abushehe · Read more

PAMBA YAANZA KIBABE NBC CHAMPIONSHIP

LIGI ya NBC Championship imeendelea leo Septemba 11 kwa mchezo mmoja kuchezwa kati ya Pamba Jiji ya Mwanza na Cosmopoilitan ya Dar uliomalizika kwa Cosmo kupoteza kwa mabao 4-0. Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza umeshuhudiwa Cosmo waliokuwa mabingwa wa First League msimu wa 2022-2023 wakienda mapumziko wakiwa wameruhusu mabao matatu. “Hii…

Honest Mwanitega · Read more

NBC CHAMPIONSHIP YAPAMBA MOTO

LIGI ya NBC Championship imeendelea Leo Septemba 10 kwa michezo minne kuchezwa kwenye mikoa mitatu tofauti. Mchezo wa mapema saa 8:00 mchana ulizikutanisha TMA na Stand United katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na kumalizika kwa suluhu. Mchezo mwengine ulizikutanisha Mbuni na Biashara United saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha…

Honest Mwanitega · Read more

NBC CHAMPIONSHIP KUENDELEA TENA LEO.

PAZIA la Ligi ya NBC Championship lilifunguliwa rasmi jana septemba, 9 kwa michezo mitatu kuchezwa. Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa michezo minne kati ya TMA na Stand United kwenye uwanja Sheikh Amri Abeid,Arusha saa 8:00 mchana. Mchezo wa pili utazikutanisha Ken Gold dhidi ya Transit Camp uwanja wa Sokoine, Mbeya saa 10:00 alasiri. Mchezo…

Honest Mwanitega · Read more

WARATIBU ‘WANOLEWA’ DAR.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) leo Septemba 9, imeendesha semina ya waratibu wa michezo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Benjamin Mkapa Dar es saalam. Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwaongezea ufanisi katika kusimamia michezo mbalimbali ya kimashindano iliyo chini ya TFF na TPLB.…

Honest Mwanitega · Read more

NBC CHAMPIONSHIP KUANZA RASMI LEO

PAZIA la Ligi ya NBC Championship msimu wa 2023/2024 linafunguliwa rasmi leo Septemba 9 kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja mbalimbali. Mchezo wa kwanza wa ufunguzi utazikutanisha Mbeya City dhidi ya Green Warriors saa 10:00 alasiri katika uwanja wa Sokoine, Mbeya mchezo wa pili utazikutanisha Mbeya Kwanza dhidi Polisi Tanzania saa 10:00 alasiri katika Uwanja…

Honest Mwanitega · Read more

YANGA YAIPIGISHA ‘KWATA’ JKT.

TIMU ya Yanga imeshinda mchezo wa pili mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufunga mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania. Mabao ya Stephane Ki Aziz, Kenedy Musonda, Kouasi Yao, na Maxi Nzengeli aliyefunga mawili yametosha kuiweka Yanga nafasi ya kwanza msimu huu ikiwa bingwa mtetezi kwa kufikisha alama sita. Mpaka sasa timu ya…

Honest Mwanitega · Read more