News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

COASTAL, JKT KUANZA NYUMBANI LEO LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC inarejea leo Septemba 29 kwa michezo miwili kuchezwa kwenye mikoa ya Tanga na Shinyanga. JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga saa 10 alasiri huku ukiwa mchezo wa kwanza wa JKT Tanzania kucheza nyumbani tangu kupanda Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa…

Yahaya Abushehe · Read more

MASHUJAA, YANGA MILANGO MIGUMU

TIMU ya Mashujaa ya mkoani Kigoma na Yanga ya Dar zimetimiza michezo mitatu ya Ligi Kuu ya NBC bila kuruhusu bao lolote. Yanga imecheza michezo mitatu nyumbani ikikusanya alama zote tisa na kuongoza msimamo wa ligi pasipo kuruhusu bao huku ikifunga mabao 11 ambapo tisa kati ya hayo yamefungwa kipindi cha pili. Mashujaa iliyopanda daraja…

Honest Mwanitega · Read more

SIMBA, AZAM HAZIKAMATIKI

Ligi Kuu ya NBC imeendelea leo Septemba 21 kwa michezo miwili kuchezwa katika viwanja viwili na kushuhudiwa Simba wakiifunga Coastal Union ya Tanga mabao 3-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani Uhuru mkoani Dar es salaam. Mabao yote matatu ya Simba yamefungwa na mchezaji Jean Baleke huku akiingia katika rekodi ya kuwa mchezaji wa pili kufunga…

Yahaya Abushehe · Read more

LIGI KUU KUENDELEA LEO.

MZUNGUKO wa tatu wa Ligi Kuu ya NBC unatarajiwa kutamatika leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye viwanja viwili tofauti vya mkoa wa Dar es Salaam. Saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Uhuru, Dar timu ya Simba iliyoshinda michezo yote miwili mpaka sasa itakuwa mwenyeji wa Coastal Union ya Tanga ambayo bado haijapata ushindi katika mchezo…

Honest Mwanitega · Read more

TMA, KEN GOLD, COPCO ZAPETA NBC CHAMPIONSHIP

TIMU za TMA ya Arusha, Ken Gold ya Mbeya na Copco FC ya Mwanza zimefanikiwa kushinda michezo yao kwenye Ligi ya NBC Championship kwa mara ya kwanza msimu huu. TMA ilicheza mapema saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na kushinda 1-0 dhidi ya Biashara ya Mara. Ushindi huo umeifanya TMA kufikisha…

Honest Mwanitega · Read more

KMC YAANZA VYEMA NYUMBANI

TIMU ya KMC ya Dar imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC kwa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania ikicheza katika uwanja wake wa Uhuru, Dar. Awesu Awesu na Waziri Junior ndio waliofunga mabao mawili na kuifanya JKT Tanzania kuwa timu iliyoruhusu mabao mengi mpaka sasa kwenye Ligi kuu ya NBC (7)…

Honest Mwanitega · Read more

POLISI YAONESHA MAKALI, PAMBA HAIKAMATIKI

TIMU ya Polisi Tanzania imepata ushindi wa kwanza kwenye Ligi ya NBC Championship dhidi ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0. Ushindi huo ulihakikishwa mapema dakika ya 15 kwa bao la Denis Mushi na kufanya Ruvu Shooting kupoteza mchezo wa pili mfululizo baada ya kufungwa dhidi ya FGA Talents mabao 2-1 katika mchezo wa ufunguzi. Pamba…

Honest Mwanitega · Read more

DODOMA, MTIBWA HAKUNA MBABE

Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma umemalizika kwa sare ya bao moja. Bao la Mtibwa Sugar lilifungwa na Abdul Hilary dakika ya 18 huku la Dodoma Jiji likifungwa na Emmanuel Martin dakika ya 38. Dakika ya 25 mchezo ulilazimika kusimama baada ya…

Yahaya Abushehe · Read more

TABORA UTD YATAMBA

Mkoani Tabora Tanzania Prisons imepoteza mchezo wa pili mfululizo dhidi ya Tabora United kwa mabao 3-1. Tabora UTD iliyopoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Azam kwa mabao 4-0 imepata ushindi huo wa kwanza kwa mabao ya John Ben aliefunga mawili na Erick Okutu huku bao la Prisons likifungwa na Samson Mbangula. Prisons imeruhusu mabao sita…

Honest Mwanitega · Read more