News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

LIGI KUU YA NBC KUREJEA LEO.

BAADA ya kusimama kwa takribani wiki tano Ligi Kuu ya NBC inatarajiwa kurejea leo Januari 16 kwa mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma kati ya timu ya Dodoma jiji itakayokuwa mwenyeji wa Singida Black Stars. Dodoma Jiji iliyoanza vibaya msimu huu imeshinda mchezo mmoja pekee wa Ligi Kuu ya NBC kwenye michezo nane iliyocheza…

Honest Mwanitega · Read more

YOUNG AFRICANS YAANZA KIBABE 2026.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya NBC timu ya Young Africans imeanza mwaka 2026 kibabe kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga timu ya Azam FC kwa mikwaju ya penati 5-4. Mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkali ilishuhudia timu hizo zikitoka suluhu ndani ya dakika 90 huku mchezaji wa Young Africans Pacome…

Honest Mwanitega · Read more

NBC CHAMPIONSHIP YANOGA.

IKIKAMILISHA mizunguko 14 Ligi ya Championship ya NBC imeendelea kuleta msisimko zaidi kutokana na ushindani wa timu zikipambana kupanda Ligi Kuu ya NBC huku nyingine zikipambana kusalia kwenye ligi hiyo kwa msimu unaofuata. Utamu wa ligi hiyo upo zaidi kwenye nafasi ya kwanza na ya pili ambapo timu ya Geita Gold inashikilia usukani na Kagera…

Honest Mwanitega · Read more

TAARIFA YA KAMATI YA SAA 72

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Desemba 15, 2025 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo; Ligi Kuu ya NBC Mechi Namba 032: Singida BS FC 1-3 TRA United FC Mchezaji Khalid Aucho wa klabu ya Singida BS ya…

Yahaya Abushehe · Read more

NASSOR IDRISSA MWENYEKITI MPYA BODI YA LIGI.

NASSOR Idrissa ‘Father’ amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) baada ya kupata kura saba (7) dhidi ya kura sita (6) za mpinzani wake CPA Hosea Lugano kwenye uchaguzi uliofanyika jana Novemba 29, 2025 katika Hotel ya Golden Tulip, Masaki Jijini Dar Es Salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari Nassor alisisitiza chini…

Yahaya Abushehe · Read more

KAGERA SUGAR KUPINDUA MSIMAMO LEO ?

Kagera Sugar inashuka Dimbani hii leo Novemba 22 kuwakabili Polisi Tanzania kwenye muendelezo wa Ligi ya Championship ya NBC 2025/2026 mchezo utakao chezwa kwenye uwanja wa Kaitaba kuanzia saa 10:00 alasiri. Kagera Sugar inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ya NBC ikiwa na alama 13 sawa na Geita Gold inayoshika nafasi…

Yahaya Abushehe · Read more

HAWA HAPA WAKALI WA ‘GUU’ LA KULIA KWENYE LIGI KUU YA NBC.

WAKALI wa kutumia mguu wa kulia katika kufunga mabao ndani ya Ligi Kuu ya NBC wanazidi kuongezeka kadri Ligi inavyozidi kuendelea ikiwa ni mzunguko wa sita wa Ligi . Maxi Nzengeli mchezaji anaecheza eneo la kiungo katika timu ya Young Africans amefanikiwa kuifungia mabao mawili timu yake akitumia ufundi wa mguu wake wa kulia na…

Cynthia Michael · Read more

NANI KUSHIKA USUKANI WA KILELE CHA MSIMAMO WA LIGI KUU YA NBC LEO ?

LIGI KUU ya NBC inarejea Leo Novemba 8 kwa michezo miwili kupigwa kwenye mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam baada ya kusimama kwa muda kwasababu ya changamoto za kiuendeshaji zilizotokana na sababu za kiusalama na Miongozo yake. Mkoani Mwanza Pamba Jiji itaialika Singida Black Stars saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa CCM Kirumba,…

Yahaya Abushehe · Read more

PRISONS WABABE WA MBEYA DABI LIGI KUU YA NBC

TIMU ya Tanzania Prisons imeendeleza ubabe wake katika mchezo wa dabi ya Jiji la Mbeya baada ya kuifunga timu ya Mbeya City mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa Uwanja wa KMC mkoani Dar es Salaam jana Oktoba 21. Mchezo huo ulianza majira ya saa 10:00 alasiri ambapo timu zote zilikuwa zikipambana kupata…

Loveness Bernard · Read more