News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

MTIBWA SUGAR YASOGEA NAFASI YA NNE LIGI KUU YA NBC

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa mchezo mmoja uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma na kushuhudia Mtibwa sugar ikifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City. Mtibwa Sugar ilianza mchezo kwa kasi na dhamira ya kutafuta ushindi mapema na juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 27 baada ya George Chota…

Cynthia Michael · Read more

YOUNG AFRICANS ‘YAICHAPA’ MASHUJAA LIGI KUU YA NBC.

Young Africans imeendelea kuonyesha ubora wao katika Ligi Kuu ya NBC ilipokutana na Mashujaa katika wa uwanja KMC Complex baada ya kuichapa Mashujaa mabao 6-0. Kikosi cha Young Africans kilitawala mchezo kuanzia dakika ya kwanza hadi mwisho huku wachezaji sita wakiandika majina yao kwenye orodha ya wafungaji. Bao la kwanza lilifungwa mapema dakika ya 8…

Cynthia Michael · Read more

SIMBA YABANWA NYUMBANI LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Simba imeshindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa pili mfululizo baada ya kulazimishwa sare ya bao moja na timu ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam. ‘Mnyama’ alikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ellie Mpanzu mapema kipindi cha kwanza kabla ya Mtibwa kusawazisha kupitia kwa Magata Fredrick bao…

Honest Mwanitega · Read more

AZAM YA IBENGE NI MOTO WA KUOTEA MBALI LIGI KUU YA NBC.

TIMU ya Azam yenye maskani yake kwenye uwanja wa Azam Complex imekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu ikiwa haijapoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu ya NBC hadi sasa. Mchezo uliopita Azam ilishinda dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa nyumbani kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Yahya Zayd, Feisal Salum na Jephte Kitambala huku mabao…

Honest Mwanitega · Read more

NBC CHAMPIONSHIP YAFIKA PATAMU.

IKIKAMILISHA mizunguko 15 Ligi ya NBC Championship imepamba moto timu zote zikiwa zimecheza michezo 15 huku zikisaliwa na michezo 15 kufunga msimu. Geita Gold inaongoza mbio za ubingwa ikiwa na alama 37 baada ya kushinda michezo 11 huku ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote hadi sasa. Kagera Sugar inashika nafasi ya pili ikiwa na…

Honest Mwanitega · Read more

AZAM, COASTAL WANA KIKAO LIGI KUU YA NBC LEO.

MATAJIRI wa Chamazi timu ya Azam leo itakuwa na kibarua cha kusaka alama tatu muhimu nyumbani dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuanza mwaka 2026 vibaya baada ya kupoteza kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Young Africans Azam itavaana na Coastal inayoshika…

Honest Mwanitega · Read more

DODOMA, SINGIDA ZATOSHANA NGUVU LIGI KUU YA NBC.

UKIWA mchezo wa kwanza unaorejesha ladha za Ligi Kuu ya NBC baada ya kusimama kwa takribani wiki tano umeshuhudia timu za Dodoma Jiji na Singida Black stars zikimaliza kwa sare ya bao moja na kugawana alama kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua ulishuhudia mabao ya timu zote mbili yakipatikana…

Honest Mwanitega · Read more

ILULU, KIGAMBONI KINAWAKA LEO NBC CHAMPIONSHIP.

LIGI ya Championship ya NBC inatarajiwa kuendelea leo kwa mzunguko wa 15 huku viwanja vya Ilulu, Lindi na TFF Center Kigamboni vikitarajiwa kutimua vumbi leo. Bigman ya Lindi itakuwa mwenyeji wa Geita Gold inayoshika usukani wa Ligi ya Championship ya NBC kwenye uwanja wa Ilulu huku timu ya Bigman ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kulazimishwa…

Honest Mwanitega · Read more