News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

MBEYA DERBY NDANI YA DAR LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC inatarajiwa kushuhudia mchezo kati ya Mbeya City na Prisons (Mbeya Derby) kwenye uwanja wa KMC Complex kwa mara ya kwanza ukipigwa mkoani Dar es Salaam huku timu zote asili yake ikiwa ni mkoani Mbeya. Hii inatokea baada ya timu ya Mbeya City kuuchagua uwanja wa KMC kama uwanja wake wa nyumbani…

Honest Mwanitega · Read more

NBC CHAMPIONSHIP KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO

LIGI ya NBC Championship inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye mikoa ya Kagera na Arusha. Majira ya saa 10:00 alasiri Kagera Sugar iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu ya NBC inatarajiwa kucheza karata yake ya kwanza leo kwenye uwanja wa Kaitaba, Kagera dhidi ya Transit Camp ili kutafuta nafasi ya kurejea kwa…

Honest Mwanitega · Read more

DIARRA,AHMAD WANG’ARA TUZO ZA SEPTEMBA.

GOLIKIPA wa timu ya Young Africans, Djigui Diarra ameng’ara baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2025/2026, huku Ahmad Ali wa JKT Tanzania, akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo. Diarra alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiwashinda Anthony Tra Bi wa Singida…

Loveness Bernard · Read more

SIMBA YAPAA KILELENI, JKT, AZAM ZATOSHANA NGUVU LIGI KUU YA NBC

TIMU ya Simba imepaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuichapa timu ya Namungo mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Simba ilifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika mbili kabla ya kipindi cha kwanza kutamatika kupitia kwa Karaboue Chamou kwa kichwa baada ya mpira wa kona uliopigwa…

Cynthia Michael · Read more

SINGIDA BLACK STARS YAPAA KILELENI MSIMAMO WA LIGI KUU YA NBC.

SINGIDA Black Stars imepanda kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Mashujaa kwenye uwanja wa KMC. Bao pekee la Singida BS limefungwa na mchezaji Elvis Rupia raia wa Kenya dakika ya 45+5 ya mchezo. Ushindi huo unaifanya Singida BS kufikisha alama…

Yahaya Abushehe · Read more

YOUNG AFRICANS,AZAM ZAANZA KIBABE LIGI KUU YA NBC.

TIMU za Young Africans na Azam zimeanza vyema msimu wa 2025/2026 baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yao ya kwanza kwenye Ligi Kuu ya NBC iliyochezwa jana Septemba 24, kwenye viwanja vya Benjamin Mkapa na Azam Complex, Dar es Salaam. Mchezo wa kwanza saa 1:00 usiku uliishuhudia Young Africans ikiikaribisha Pamba Jiji kwenye uwanja…

Cynthia Michael · Read more

COASTAL UNION YASHINDWA KUFURUKUTA IKIWA NYUMBANI

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa mchezo mmoja kati ya Coastal union na JKT Tanzania kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kushuhudia Coastal Union ikishindwa kutamba baada ya kufungwa mabao 1-2. Mchezo ulianza kwa kasi na ilikuwa Coastal Union iliyokuwa ya kwanza kuandika bao dakika ya 21 kwa shuti kali la mchezaji Athumani Makambo. Bao…

Cynthia Michael · Read more

LIGI KUU YA NBC YAENDELEA KUSHIKA KASI

LIGI kuu ya NBC imeendelea kushika kasi kwa michezo mitatu iliyochezwa kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Tanzanite Kwaraaa mkoani Manyara na Majaliwa mkoani Lindi. Mchezo wa kwanza uliopigwa saa 8 kamili mchana ulizikutanisha timu za Fountain gate na Mbeya city na kushuhudia Fountain Gate ikipoteza kwa bao moja lililofungwa na Habib Kyombo…

Cynthia Michael · Read more