News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

GEITA ‘WAKALI’ WA KUTUPIA NBC CHAMPIONSHIP.

Geita Gold imeendelea kuonyesha ‘ubabe’ wake kwenye Ligi ya Championship ya NBC baada ya kutupia mabao 60 ikiwa ni idadi kubwa hadi sasa msimu wa 2025/2026. Timu hiyo iliyopo katika mbio za kurejea Ligi Kuu ya NBC baada ya kushuka msimu wa 2023/2024 ikiwa ni takribani misimu miwili ikicheza Ligi ya Championship huku ikiongoza msimamo…

Loveness Bernard · Read more

CHIRWA HAKAMATIKI NBC CHAMPIONSHIP.

MSHAMBULIAJI wa timu ya Kagera Sugar Obrey Chirwa hakamatiki hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya kuwa kinara kwa kufunga mabao akiwa nayo 16 hadi sasa ndani ya Ligi ya Championship ya NBC. Ligi hiyo imeshachezwa mizunguko 27 huku ikiwa imesalia mizunguko mitatu ili Ligi hiyo kufikia ukingoni ambapo pia mchezaji huyo ameisaidia timu yake kuwa…

Loveness Bernard · Read more

‘WALINDA LANGO’ LA AZAM NI MOTO WA KUOTEA MBALI LIGI KUU YA NBC.

Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 imeendelea kushuhudia ushindani mkubwa si tu katika ufungaji wa mabao, bali pia katika uimara wa safu za ulinzi huku takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa Azam ndiyo timu iliyocheza michezo mingi zaidi bila kuruhusu bao, ikifanikiwa kutofungwa katika michezo 20 hadi sasa. Azam imeonyesha nidhamu kubwa langoni chini…

Cynthia Michael · Read more

YOUNG AFRICANS,AZAM ZATAKATA NYUMBANI LIGI KUU YA NBC.

Ligi Kuu ya NBC imeendelea kushika kasi huku vigogo wakionyesha makali yao ambapo timu ya Young Africans na Azam zikifanikiwa kupata alama tatu muhimu kwenye viwanja vyao vya nyumbani. Katika Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam mchezo wa kwanza uliwakutanisha mabingwa watetezi Young Africans dhidi ya Namungo na kushuhudia ‘Wananchi’ wakipata ushindi wa…

Cynthia Michael · Read more

LIGI KUU YA NBC YAENDELEA KUTIMUA ‘VUMBI’.

Ligi Kuu ya NBC imeendelea kutoa ushindani mkubwa huku timu mbalimbali zikipigania nafasi za juu na kujinusuru kwenye maeneo ya hatari na kumalizia msimu huu. Mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar iliwakaribisha JKT katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro na mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2. Mtibwa ilipata mabao yake kupitia Haroun Lwawatwa…

Cynthia Michael · Read more

LIGI KUU YA NBC YAZIDI KUSHIKA KASI.

LIGI Kuu ya NBC imeendelea kwa michezo mitatu iliyotoa ushindani mkubwa huku Simba pekee ikifanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu na michezo mingine kutamatika kwa sare. Katika Uwanja wa Mej. Jen Isamuhyo, Dar es Salaam, mchezo wa mapema ulikuwa kati ya JKT Tanzania na Fountain Gate uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo…

Cynthia Michael · Read more

ISAMUHYO, MKWAKWANI, MAJALIWA ‘KUWAKA MOTO’ LIGI KUU YA NBC.

Ligi Kuu ya NBC inaendelea kwa michezo mitatu muhimu ambayo inaweza kubadilisha nafasi za timu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC. Mchezo wa kwanza utaanza saa 10:00 alasiri katika Uwanja wa Mej. Jen. Isamuhyo ambapo JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Fountain Gate. JKT Tanzania wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa nafasi ya 6…

Cynthia Michael · Read more

CLATOUS CHAMA NA REKODI MPYA LIGI KUU YA NBC.

‘STAA’ wa Simba, Clatous Chama ameendelea kuandika historia ndani ya LIGI KUU NBC baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa mchezo(Man of the Match) mara nne mfululizo katika msimu wa 2025/2026. Kiungo huyo raia wa Zambia ameonyesha kiwango cha juu katika mechi za hivi karibuni, akiongoza safu ya ushambuliaji…

Cynthia Michael · Read more

MZUNGUKO WA 23 WATAMATIKA KIBABE LIGI KUU YA NBC.

LIGI Kuu ya NBC jana ilitoa burudani ya kiwango cha juu huku mashabiki wakishuhudia jumla ya mabao 13 yakifungwa kwenye viwanja tofauti. Mchezo wa mapema kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya uliwakutanisha ‘Maafande’ wa Tanzania Prisons waliopata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya. George Mpole aliibeba timu hiyo…

Honest Mwanitega · Read more