News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

NADO, FEISAL VINARA WA KUTUMIA ‘GUU’ LA KULIA.

WACHEZAJI wa timu ya Azam, Iddi Selemani na Feisal Salum, wanashikilia usukani kwenye orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi kwa kutumia mguu wa kulia katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 hadi sasa baada ya kila mmoja kufunga mabao nane. Nyota hao wa Azam wamekuwa na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya…

Cynthia Michael · Read more

GEITA ‘WANATUPIA’ MABAO TU.

Geita Gold imeendelea kuonyesha ‘ubabe’ wake kwenye Ligi ya Championship ya NBC baada ya kutupia mabao 63 ikiwa ni idadi kubwa hadi sasa msimu wa 2025/2026. Timu hiyo iliyopo katika mbio za kurejea Ligi Kuu ya NBC baada ya kushuka msimu wa 2023/2024 ikiwa ni takribani misimu miwili ikicheza Ligi ya Championship huku ikiongoza msimamo…

Loveness Bernard · Read more

‘FEITOTO’ KINARA WA MABAO YA ‘UTOSI’ LIGI KUU YA NBC.

LICHA ya kujulikana zaidi kwa uwezo wao wa kucheza mpira wa chini na kutengeneza nafasi za kufunga, baadhi ya nyota wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 wameonyesha ubora mkubwa wa kufunga mabao kwa kichwa. Kiungo mshambuliaji wa Azam na raia wa Tanzania Feisal Salum (Feitoto), ndiye kinara wa orodha hiyo akiwa amefunga mabao…

Cynthia Michael · Read more

CHIRWA AJIPATA CHAMPIONSHIP.

MSHAMBULIAJI wa timu ya Kagera Sugar Obrey Chirwa amejipata baada ya kuzidi kutupia mabao kwa kufikisha 17 hadi sasa ndani ya Ligi ya Championship ya NBC. Ligi hiyo imeshachezwa mizunguko 28 huku ikiwa imesalia mizunguko miwili ili Ligi hiyo kufikia ukingoni ambapo pia mchezaji huyo ameisaidia timu yake kuwa nafasi ya pili kwenye msimamo huku…

Loveness Bernard · Read more

GEITA, KAGERA WAREJEA LIGI KUU YA NBC.

TIMU za Geita Gold na Kagera Sugar zimerejea rasmi Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027 baada ya kufikisha alama ambazo hazitaweza kufikiwa na timu zingine katika michezo ya Ligi ya Championship ya NBC iliyosalia. Geita Gold imefikisha alama 71 baada ya kuifunga Songea United mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa leo na kufanikiwa kurejea Ligi…

Loveness Bernard · Read more

MZUNGUKO WA 28 NBC CHAMPIONSHIP KUTOA TASWIRA NZIMA LEO

MZUNGUKO wa 28 wa Ligi ya Championship ya NBC unaendelea leo katika viwanja nane nchini ambapo michezo hiyo itachezwa saa kumi alasiri huku michezo miwili ikiwa mbashara kwenye chaneli ya Ligi Kuu Tv inayopatikana Youtube na Fifa+. Geita Gold itaikaribisha timu ya Songea United katika uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita ambapo pia timu ya Geita…

Loveness Bernard · Read more

‘WAZEE’ WA ‘MAKOMBORA’ YA LIGI KUU YA NBC.

Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 imeendelea kushuhudia mabao ya kuvutia kutoka nje ya eneo la hatari, huku baadhi ya nyota wakionyesha uwezo mkubwa wa kupiga mashuti sahihi yanayowapa mashabiki burudani ya kipekee. Kinara wa orodha hiyo ni mshambuliaji wa Azam Idd Seleman ambaye hadi sasa ameweka kambani mabao matano akifunga kutoka nje ya…

Cynthia Michael · Read more

OKELLO KINARA WA MABAO YA MGUU WA KUSHOTO LIGI KUU YA NBC.

MSHAMBULIAJI wa Young Africans raia wa Uganda Allan Okello ameendelea kuonyesha ubora wake katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26 baada ya kuongoza kwenye orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi kwa kutumia mguu wa kushoto. Nyota huyo anaongoza kwa mabao 10 ya mguu wa kushoto akithibitisha uwezo wake mkubwa wa kumalizia mashambulizi na…

Cynthia Michael · Read more