News

Announcements, match reports and updates from the Tanzania Premier League Board.

HAWA HAPA WAKALI WA MECHI ZA NYUMBANI NBC CHAMPIONSHIP.

JUMLA ya michezo 184 ya Ligi ya NBC Championship imechezwa kwenye viwanja mbalimbali kwenye mikoa 11 tofauti ikihusisha michezo ya nyumbani na ugenini kwa kila timu shiriki. Biashara United inaongoza msimamo kwa timu zilizoshinda mechi nyingi nyumbani ikifanya hivyo mara 10 kwenye michezo 12 iliyocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani Karume mkoani Mara. Mbeya…

Yahaya Abushehe · Read more

KENGOLD HASHIKIKI NBC CHAMPIONSHIP.

MZUNGUKO wa 23 wa Ligi ya NBC Championship umemalizika na kushuhudiwa jumla ya mabao 15 yakifungwa kwenye michezo 8. kenGold inaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo ikıwa na alama 53 tofauti ya alama nne na timu ya Biashara United huku kila timu ikisalia na michezo saba. Biashara United inashika nafasi ya pili…

Yahaya Abushehe · Read more

KENGOLD, BIASHARA VINARA WA USHINDI NBC CHAMPIONSHIP.

TAYARI mizunguko 22 ya Ligi ya NBC Championship sawa na michezo 176 imeshachezwa na Kushuhudiwa jumla ya mabao 401 yakifungwa. KenGold na Biashara United ndiyo timu zinazoongoza kwa kushinda michezo mingi kwenye Ligi ya NBC Championship zikifanya hivyo mara 15 kila mmoja huku KenGold ikifunga mabao 37 na kuruhusu mabao 12 na kufikisha alama…

Yahaya Abushehe · Read more

RUVU YAONJA RADHA YA USHINDI NBC CHAMPIONSHIP, PAMBA YABANWA MABATINI.

MICHEZO mitatu ya Ligi ya NBC Championship mzunguko wa 21 imechezwa kwenye mikoa mitatu tofauti. Ruvu Shooting kwa mara ya kwanza ndani ya NBC Championship inaondoka na alama tatu baada ya kuifunga Mbuni mabao 2-1 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma mchezo uliopigwa saa 8:00 mchana, Ruvu Shooting imewachukua michezo 21 kusubiri alama tatu…

Yahaya Abushehe · Read more

DODOMA, PWANI, SHINYANGA NBC CHAMPIONSHIP INAPIGWA LEO.

NBC Championship mzunguko wa 21 inaendelea leo kwa michezo mitatu kuchezwa kwenye MIKOA ya Dodoma, Pwani na Shinyanga. Mkoani Dodoma Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Mbuni saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Jamhuri. Ruvu Shooting ipo nafasi ya mwisho kwenye msimamo na alama nne huku Mbuni ikiwa nafasi ya sita na alama 37. Mkoani…

Yahaya Abushehe · Read more

MZIZIMA DERBY HAKUNA MBABE.

MCHEZO wa Ligi Kuu ya NBC Simba dhidi ya Azam umemalizika kwenye uwanja wa CCM KIRUMBA mkoani Mwanza kwa sare ya Bao 1. Prince Dube anaendelea kuwa mwiba mkali kwa Simba kwenye michezo ya hivi karibuni kutokana na kufunga kwenye michezo mfululizo wanapokutana na Simba hii ni baada ya kufunga goli la uongozi kwa…

Yahaya Abushehe · Read more

MZIZIMA DERBY KUPIGWA LEO CCM KIRUMBA.

LIGI Kuu ya NBC inaendelea Leo kwa mchezo mmoja kuchezwa kati ya Simba na Azam “Mzizima Derby” kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza saa 10:00 alasiri. Simba inaingia kwenye mchezo Huu ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo na alama 29 kwenye michezo 12 huku Azam ikiwa nafasi ya pili ikiwa na alama 31…

Yahaya Abushehe · Read more

KENGOLD KUENDELEA KUJICHIMBIA KILELENI NBC CHAMPIONSHIP LEO ?

NBC Championship mzunguko wa 21 unaanza Leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye kwenye mikoa miwili ya Pwani na Morogoro. Mkoani Pwani Pan African itaikabili KenGold saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa Mabatini, KenGold inaongoza msimamo wa Ligi ikiwa na alama 44 kwenye michezo 20 iliyocheza mzunguko huu unaweza kuamua ni nani atakayeongoza usukani wa…

Yahaya Abushehe · Read more